THE BEST BLOG IN TOWN

Powered by Blogger.

Text

RSS

Mwanasheria Mkuu awaasa wanasheria kuepuka rushwa

24th July 2013


Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werrema

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werrema, amewaasa wanasheria nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa wawapo katika majukumu yao ya kazi. Werrema alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya wanasheria wapya wa serikali ambao baada ya mafunzo hayo ya muda mfupi kuwajengea uwezo wanatarajiwa kupangiwa vituo vipya vya kazi. Aliwataka wanasheria hao wapatao 30 kuzingatia maadili ya taaluma yao pamoja, kutenda haki na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kupotosha hukumu. Kauli ya Werema inakuja huku wimbi kubwa la ufisadi kama vile rushwa likielezwa na watafiti mbalimbali kuvifunika vyombo vya dola ikiwamo mahakama, polisi na vituo vya afya. Hivi karibuni Shirika la Utafiti la Kimataifa la Transparency la nchini Kenya, lilitoa takwimu za vitendo vya rushwa kushamiri katika maeneo hayo ya dola kwa nchi takribani 120. Baadhi ya nchi zilizoonekana kukithiri kwa vitendo hivyo vya kifisadi ni pamoja na Uganda na Tanzania.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment