THE BEST BLOG IN TOWN

Powered by Blogger.

Text

RSS

P Square feat. RickRoss – Beautiful Onyinye Remix(2012)

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

WATANZANIA WATAKIWA KUUDHAMINI UTAMADUNI WAO

Msanii wa Ras Innocent Nganyagwa akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kushoto kwake ni Afisa Habari Mkuu BASATA Bi Agnes Kimwaga.

ENDELEA ZAIDI

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Lebejo akisisitiza jambo wakati akihitimisha programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii.

Na Mwandishi Wetu Watanzania wametakiwa kuuenzi utamaduni wa makabila ambao una thamani kubwa sana, wito huu umetolewa wiki hii kwenye ukumbi wa BASATA na

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA ADDIS ABABA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Jordan Rugimbana na wa tatu toka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa Julai 16, 2012 akitokea Addis Ababa, Ethiopia, katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Saidi Mecky Sadik baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa Julai 16, 2012 akitoketa Addis Ababa, Ethiopia, katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Saidi Mecky Sadik na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa Julai 16, 2012 akitokea Addis Ababa, Ethiopia, katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa Julai 16, 2012 akitokea Addis Ababa, Ethiopia, katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Saidi Mecky Sadik na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa Julai 16, 2012 akitokea Addis Ababa, Ethiopia, katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Afrika. (PICHA NA IKULU)

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

RAIS WA LIBERIA ELLEN SIRLEAF KUWASILI NCHINI LEO KWA ZIARA YA SIKU TATU

Rais wa Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Ben Paul - Maneno Maneno (Official Video)

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Diamonds - Liveshow Ziff (Zanzibar)

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

NEW TRACK: Poppa Ft Koba Mc - PUNDA


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Hafla ya Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa


Hafla ya Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa kuzindua kampeni ya kutangaza vivutio vya kitalii nchini Australia...Picha zaidi zinapatiaka kwenye Jumuiya Tanzanian Community of NSW Australia facebook na website.

Bodi ya Utalii Tanzania, wiki iliyopita imezindua kampeni ya kutangaza vivutio vya kitalii kwa wageni nchini Australia. Hafla ya uzinduzi huo uliongoza na mkurugenzi wa bodi bwana Aloyce Kilua na kuhudhuriwa na balozi wa Japan anayewakilisha pia Australia, New Zealand na Korea Kusini Mh Salome Sijaona, ilifanyika katka hotel ya Novotel mjini Sydney huku wenyeji wa hafla hiyo wakiwa ni Jumuiya ya Watanzania NSW Australia na kusimamiwa na katibu wake Bw Frank Mtao na Connie Offeh!


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Pambano la mafahari wawili! Wema vs Wolper



WEMA

Jackline Wolper akisali kabla ya pambano

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Diamond kuigiza kwenye filamu mpya ya Steps Entertainment


Mwanamuziki wa Bongo Flava, Diamond anatarajia kuigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu itakayotayarishwa na kampuni ya Selles Business Inc na kusambazwa na Steps Entertainment Limited. Akiongea kwa simu na Bongo5 jana, mtunzi na muongozaji wa filamu hiyo Selles Mapunda amesema, “mwishoni mwa mwaka jana nilikuwa na wazo la kufanya sinema, nilifanya kikao na Diamond pale Lions Hotel Sinza, tukaongea biashara nyingine, tukaenda kwenye show moja Mombasa na yeye lakini pia likaja wazo la kufanya naye sinema.” Mapunda amesema ameifanyia kazi filamu hiyo kwa zaidi ya miezi saba na sasa yupo kwenye hatua ya mwisho ya kuikamilisha. Amesema kwenye filamu hiyo ya Diamond atawashangaza watu kama ilivyokuwa kwenye filamu ya Crazy Tenant aliyoigiza msanii Peter Msechu na Wema Sepetu. “Sinema ni tamu,tamu sana nawahakikishia kwamba mkiiona mtasema kwamba Diamond huyu sio yule wa muziki, huyu ni Diamond mwingine wa movie.” Ameongeza kuwa mpaka sasa hajaipa jina filamu hiyo japo Diamond alikuwa na wazo la kuiita filamu hiyo ‘Nimpende Nani’ kutokana na wimbo alioufanya wenye jina hilo na kuongeza kuwa anategemea kutangaza jina la movie hiyo wiki ijayo. Muongozaji huyo wa filamu amesema ilikuwa rahisi kugundua kipaji cha Diamond katika uigizaji kutokana uzoefu mkubwa alionao kwenye tasnia ya filamu. “Mimi ni mwalimu, professional wa sinema,mimi ni mzalishaji wa wasanii wa sinema Tanzania. Mimi nimesoma sinema, tena nimesoma Nigeria kwa wamakonde kabisa wanaojua sinema zinavyofanywa . Kiulewa wangu na uwezo wangu,Diamond anaweza kufanya kitu ambacho mtu hata mmoja hakufikiria” Amedokeza kuwa katika filamu hiyo Diamond ambaye ni mhusika mkuu ataigiza na muigizaji mmoja wapo kati ya Wema Sepetu ama Jokate Mwegelo. “Ni Wema na Jokate, lakini mmoja anafanya mmoja hafanyi, sikuambii ni nani leo” Mapunda amesema katika filamu hiyo Diamond atamlipa shilingi milioni tano. “Sinema zangu zote huwa wasanii nawalipa kwanza kabla hawajaanza sinema, nawalipa advance na wanapomaliza nawalipa hela. Sijafanya sinema zile za kukopeshana.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Shilole feat. Kitokololo & Rich Mavoko - Viuno tucheze (Official Video)

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Mama yake Lil Wayne Aolewa


Lil-Wayne-gushing-over-his-mother

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Figo za Dk Ulimboka zaanza kufanya kazi


Waandishi Wetu AFYA ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imeendelea kuimarika baada ya kupata matibabu nchini Afrika Kusini na sasa figo zake zimeanza kufanya kazi.Dk Ulimboka alipelekwa nchini huko mwishoni mwa wiki baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kiasi cha kusababisha figo zake kushindwa kufanya kazi.Katibu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Rodrick Kabangila alisema Dar es Salaam jana kwamba, hali ya Dk Ulimboka imeimarika na kuwaomba Watanzania wamuombee apone haraka.“Taarifa tulizozipata kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba, hali ya Dk Ulimboka imezidi kuimarika tofauti na alivyokwenda, figo zimeanza kufanya kazi ingawa kwa polepole na amefanyiwa vipimo vingine,” alisema Dk Kabangila na kuongeza:“Pia ameanza kuzungumza, anawatambua watu vizuri na zaidi amewaomba Watanzania wamuombee apone haraka.” Awali, chanzo kimoja cha habari kilidokeza kwamba hali ya Dk Ulimboka imeimarika kutokana na kupatiwa huduma za matibabu kwa haraka kwa kufanyiwa pamoja na vipimo vingine, kile cha usafishaji damu na figo (Dalysis), mara kwa mara. Kabla ya kuondoka nchini, Dk Ulimboka alifanyiwa usafishaji huo mara mbili. Madaktari walisema kuwa, kipimo hicho kililenga kupunguza kiwango cha sumu iliyoonekana kwenye damu, ambayo haikutambulika mara moja kama ilitengenezwa ndani ya mwili au vinginevyo kwa kuwa hakuna kipimo cha kubaini tatizo hilo nchini. Migomo hospitalini Licha ya huduma kurejea taratibu katika baadhi ya hospitali nchini, mgomo wa madaktari bingwa umeendelea chini kwa chini.Pia jana, Serikali imewataka madaktari wote walio katika mafunzo ya vitendo kuripoti Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ifikapo Ijumaa. Jana, wizara hiyo ilitoa taarifa ikitaka madaktari wote nchini wanaofanya mafunzo kwa vitendo (interns) ambao walipewa barua za kurudishwa wizarani, kuripoti Dar es Salaam Julai 6, mwaka huu. Mgomo wa madaktari bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umekuwa na utata baada ya kuwapo taarifa mbili zinazokinzana. Uongozi wa (MNH) kupitia kwa Msemaji wake, Aminiel Aliegaeshi umetoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari jana ukisema huduma za matibabu zinaendelea kama kawaida, lakini kwa kiwango cha kati. “Huduma hapa hospitalini zinaendelea kutolewa kwa kiwango cha kati, wagonjwa ni wachache wanaokuja kutibiwa. Madaktari Bingwa wote wameingia na kufanya kazi na Interns kumi na moja wamefanya kazi,” alisema. Jana waandishi wetu walishuhudia baadhi ya huduma zikiendelea kutolewa kama kawaida katika hospitali hiyo zikiwemo x-ray katika Taasisi ya Mifupa (Moi) na hospitali hiyo kuu. Awali, huduma hiyo na nyingine zilisimama baada ya tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka. Lakini, wakati Aliegesha akitoa taarifa hiyo, madaktari bingwa wamesisitiza kuwa wako kwenye mgomo huku msemaji wao, Dk Cathrine Mng’ong’o akitaka waandishi wa habari kulinganisha maneno hayo ya uongozi na hali halisi hospitalini hapo. “Mimi siwezi kujibu swali hilo (kama wako kwenye mgomo au wamerudi), sababu sipo katika eneo la hospitali leo, niko nyumbani. Wewe angalia kwa macho yako uone kisha linganisha maneno hayo na hali halisi,” alisema Dk Mng’ong’o.Alipoulizwa kuwa kama jana alikuwa zamu alijibu kwa kifupi kuwa madaktari bingwa hawana zamu na hufanya kazi saa 24. Madaktari hao juzi walitangaza mgomo wakitaka Serikali kuwarudisha kazini madaktari wote waliofukuzwa. Uongozi wa MNH ulisema, idara ambazo madaktari walikuwapo ni ya huduma za dharura na katika vitengo vingine ilidaiwa kuwa walifika kwa kiwango kikubwa. Katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, hali imezidi kuwa tete baada ya wagonjwa kuhamishiwa hospitali za binafsi kutokana na kuzorota kwa huduma.Mkazi wa Sakina aliyejitambulisha kwa jina moja la Manka, ambaye mtoto wake alikuwa amelazwa hospitalini hapo akisubiri upasuaji alisema, amelazimika kumhamisha mtoto wake kutokana na kukosa huduma. Hata hivyo, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Eliringia Mlay alikanusha madai ya kuwapo kwa mgomo hospitalini hapo na kusema kuwa, ulikuwapo awali lakini kwa sasa umekwisha na madaktari wanaendelea na kazi kama kawaida. Hospitali binafsi Hospitali ya TMJ imeanza kutoa huduma ya tiba kwa baadhi ya wagonjwa waliokuwa Muhimbili baada ya kuingia mkataba na Serikali ili kutoa huduma ya matibabu katika kipindi ambacho madaktari wa Serikali wapo katika mgomo. Msemaji wa Hospitali hiyo, Huzaifa Seif alisema jana kuwa wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hiyo ni wale wenye kadi za Bima ya Afya na wagonjwa walioandikiwa rufaa kutoka MNH. Hata hivyo, mmoja wa wagonjwa, Anaeli Mbasha alisema ingawa Serikali imeingia mkataba na hospitali hiyo, wagonjwa wengine wenye kipato kidogo wanashindwa kuhimili malipo. Hospitali ya Regency imekuwa na ongezeko la wagonjwa ikiaminika kuwa ni kutokana na mgomo huo wa madaktari. Mmoja wa madaktari hospitalini hapo, Dk Emmanuel Jonathan alisema wagonjwa ni wengi hasa kutoka Muhimbili. Katika Hospitali ya Aga Khan, baada ya wiki iliyopita kuwa na ongezeko la wagonjwa kwa asilimia 15, idadi hiyo imepungua kati ya jana na juzi.Mkurugenzi wa Tiba wa Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee alisema: “Ongezeko kubwa lilikuwa katika vipimo ambavyo vinapatikana katika Hospitali ya Muhimbili na hapa (Aga Khan), peke yake kwa mfano MRI (Magnetic Resonance Imaging).”

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

LULU ACHIMBA MKWARA MAHAKAMANI



MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amechimba mkwara mzito katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, Risasi Mchanganyiko linatiririka. Lulu ambaye ni mshukiwa namba moja wa kifo cha msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba, alichimba mkwara huo, juzi Julai 02, mwaka huu wakati akifikishwa mahakamani hapo, kesi yake inapoendeshwa. ATEMA CHECHE Baada ya Lulu kushuka katika gari la Magereza na kusindikizwa kwenda kizimbani na askari Magereza, alianza kumshambulia mwandishi wetu kwa maneno alipomuona amekazana kupata picha zake. “Hivi hamchoki kunifuatafuata? Kila siku Lulu, Lulu niacheni na maisha yangu! Kwani kuna kitu gani kipya tena? “Hivi nyie hamna kazi nyingine ya kufanya...baba mzima unahangaika kunifuatilia? Nimechoshwa na tabia yenu bwana,” alibwatuka Lulu bila woga. ASKARI WAPIGWA NA BUTWAA Wakati Lulu akitema cheche, askari waliokuwa ‘wakimueskoti’ walibaki wamepigwa na butwaa bila kuamini kama ni kweli Lulu ndiye aliyekuwa akizungumza kwa ujasiri mkubwa kiasi kile. Mdau mmoja aliyekuwepo mahakamani hapo, alisikika akisema: “Mh! Mwanzoni Lulu alikuwa analia kila siku, lakini sasa naona ameanza kuzoea...amekuwa mbogo huyo!” KESI YAKE NENDA RUDI Kesi ya Lulu imeonekana kuwa na mvutano mkubwa huku matumaini ya kuanza kusikilizwa yakionekana kuwa hafifu kutoka na shauri hilo kuendeshwa katika mahakama mbili tofauti. Awali, Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo, Elizabeth Kaganda, mbele ya Hakimu Agustina Mbando alisoma kesi hiyo lakini kabla ya mtuhumiwa hajajibu chochote, hakimu aliihairisha kesi hiyo. Hakimu Mbando alisema, analazimika kuhairisha kesi hiyo hadi Julai 16, mwaka huu kwa vile shauri hilo halijakamilika kwa sababu lipo Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ikijadiliwa suala la umri. Hata hivyo, mahakama kuu ilipeleka shauri hilo katika mahakama ya rufaa baada ya mawakili upande wa serikali, kupinga suala la umri wa Lulu kujadiliwa mahakamani hapo, badala yake lipelekwe katika mahakama ya rufaa. Mawakili hao walisema, kwa sasa Lulu atabaki kujulikana kuwa ana umri wa miaka 18, ambao aliandikisha yeye mwenyewe katika Kituo cha Polisi Oysterbay alipokuwa akihojiwa kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa. NDUGU, WASANII WAMTOSA Aidha, siku hiyo hakukuwa na ndugu yeyote wa Lulu wakiwemo wazazi wake aliyefika mahakamani hapo kufuatilia shauri hilo. Ukiachilia mbali hao, hata wasanii wenzake ambao wana jumuiya mbalimbali kama Bongo Movie na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) pia hawakufika kumuona mwenzao. KUMBUKUMBU MUHIMU Lulu alikamatwa Aprili 07, mwaka huu kwa madai ya kuhusika na kifo cha marehemu Kanumba, kilichotokea nyumbani kwake, Sinza - Vatican, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia siku hiyo. Kwa sasa yupo katika Gereza la Segerea huku kesi yake ikiendelea kuunguruma katika mahakama mbili tofauti; Hakimu Mkazi, Kisutu na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

ANAYEOLEWA NA BOB JUNIOR HUYU HAPA


Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Rais wa lebo ya Sharobaro Records ya jijini Dar es Salaam, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ kufunga pingu za maisha, kimwana anayetarajiwa kupika mahajumuti nyumbani kwa bosi huyo wa wasafi dunia nzima amejulikana. Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo kimoja kilichopo mjini Zanzibar, kimeidokeza Teentz.com kuwa Bob Junior huenda akafunga pingu za maisha na nyota wa filamu kutoka visiwani humo Halima Ally ‘Imma’ ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa karibu kwa kiasi kikubwa na Produza huyo kila anaikanyaga ardhi ya visiwa hivyo vya karafuu.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

DIAMOND APOKELEWA KWA MSAFARA SONGEA


Akizungumza na Teentz.com VIA 4N mara baada ya kuwasili wilayani humo, Diamond alifunguka kuwa amepata mapokezi ya ajabu ambayo hajawahi kuyaona toka alivyoanza kuwajibika ndani ya gemu ya muziki wa kizazi kipya. "Nimepokelewa kwa msafara wa magari na pikipiki nyingi kama ambavyo hupokelewa viongozi wakuu wa nchi hapa nilipo kuna watu wengi kupita maelezo ambao wamejitokeza kunipokea , hakika sijawahi kuona jambo hilo kabla, namshukuru Mungu kwa kila kinachotokea hii inanipa moyo wa kufanya kazi zaidi ili kuwafurahisha mashabiki wangu" alisema Diamond

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

GARI LA WOLPER LAKAMATWA


Jacqueline Wolper



BMW X6 ya Wolper iliyokamatwa.


Wolper akishushwa kwenye gari lake.

LILE gari la kifahari aina ya BMW X6 lenye namba za usajili T 574 BXF linalomilikiwa na staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper Masawe limedakwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa TRA ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, gari hilo la kisasa lilikamatwa Juni 28, 2012 kupitia Kampuni ya Mnada ya Majembe kutokana na sababu kadha wa kadha. SABABU ZAANIKWA Akiendelea kufunguka, afisa huyo alisema kuwa sababu ya kwanza ni kuhisiwa kuwa gari hilo liliingizwa nchini kinyemela kutokana na vielelezo vyake vya kwenye kadi kupitia kwenye vyombo vya habari, ndipo taa nyekundu ikawaka ndani ya vichwa vya maafisa wa TRA na kuanza kulifuatilia. Alidai kuwa mbali ya kuingia nchini kinyemela, lakini BMW hilo halijalipiwa ushuru zaidi ya miaka mitano iliyopita kwa mujibu wa vielelezo vyake. MPANGO WA KULIKAMATA ULIVYOSUKWA Kwa mujibu wa ofisa huyo, ili kufanikisha zoezi la kulikamata gari hilo, vijana kutoka kampuni ya Majembe waliingia mzigoni kulisaka ambapo kuna mtu alipiga kambi jirani na makazi ya Wolper, Mbezi Beach jijini Dar. Ilisemekana kuwa vijana hao walikuwa na kazi moja tu, kuhakikisha anapotoka Jack wanamfuatilia hatua kwa hatua hadi mahali atakapokwenda kupiga kambi na kulitia mikononi. “Haikuwa kazi rahisi maana muda mrefu alikuwa haonekani nalo, ndipo mpango huo ulipokuja kukamilishwa kwa njia ya kumfuatilia anapotoka kwake hadi mahali lilipokamatwa maeneo ya katikati ya Jiji la Dar,” alisema. Akaendelea kudai: “Unajua hawa mastaa wetu kuna vitu wanavifanya bila kujua madhara yake, kitendo cha Wolper kuonesha kadi ya gari kwa waandishi wa habari huku anafahamu ina mapungufu kibao ndiyo sababu kuu ya gari hilo kuanza kufuatiliwa.” MH! ETI USHURU MILIONI 70? Taarifa nyingine ya kushtua ni kwamba ilidaiwa kuwa kuwa TRA peke yake inadai Sh. milioni 70 za ushuru. “Si fedha ndogo zinazodaiwa na TRA, kwa hesabu ya harakaharaka ni zaidi ya Sh. milioni 70 ambazo zinatakiwa kulipwa.” Baada ya The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda kujiridhisha kuwa gari hilo limedakwa, lilimuendea hewani Wolper lakini hakuweza kupokea simu hadi gazeti linakwenda mitamboni.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA DKT. KACOU ATEMBELEA BANDA LA MFUKO WA FURSA SAWA KWA WOTE (EOTF).



Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akiwasili katika banda la Mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOTF) wakati wa maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.Kushoto ni Afisa Mawasaliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu.



Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa (kulia) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou (kushoto) katika banda la mfuko huo.



Mkurugenzi Mtendaji wa (EOTF ) Bw. Stephen Emmanuel (kulia) akisalmiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.



Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou akitia saini kitabu cha wageni katika banda la mfuko wa fursa sawa kwa wote (EOTF).



Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akikagua moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kutoka bara na visiwani ambao wamepewa mafunzo na mfuko huo kabla ya kushiriki maonyesho hayo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa (EOTF ) Bw. Stephen Emmanuel , Mwenyekiti wa Mfuko huo Mama Anna Mkapa pamoja na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu



Dkt. Alberic Kacou akitazama Juisi asilia ambao haijachanganywa na kemikali yoyote zinazotengenezwa na kikundi cha Wajasiriamali wa KYM'S ENTERPRISES cha Kibaha wanaopatikana katika banda la mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOSF).



Katika ziara hiyo Dkt. Alberic Kacou alikutana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (Kushoto) alipotembelea banda la mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS