THE BEST BLOG IN TOWN

Powered by Blogger.

Text

RSS

ANAYEOLEWA NA BOB JUNIOR HUYU HAPA


Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Rais wa lebo ya Sharobaro Records ya jijini Dar es Salaam, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ kufunga pingu za maisha, kimwana anayetarajiwa kupika mahajumuti nyumbani kwa bosi huyo wa wasafi dunia nzima amejulikana. Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo kimoja kilichopo mjini Zanzibar, kimeidokeza Teentz.com kuwa Bob Junior huenda akafunga pingu za maisha na nyota wa filamu kutoka visiwani humo Halima Ally ‘Imma’ ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa karibu kwa kiasi kikubwa na Produza huyo kila anaikanyaga ardhi ya visiwa hivyo vya karafuu.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment