Rais wa Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf.
Rais wa Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, anatarajiwa kuwasili
nchini tarehe 17 Julai, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Ziara
hiyo ya Mhe. Sirleaf inafuatia mwaliko wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Sirleaf ambaye atawasili siku hiyo saa 8.00 mchana katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, atapokelewa na mwenyeji
wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Akiwa hapa nchini, Mhe. Sirleaf anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo
rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 17 Julai 2012, ikifuatiwa na Dhifa ya
Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Rais Kikwete, Ikulu, Dar
es Salaam.
Aidha, Mhe. Sirleaf pia anatarajiwa kuzindua Ofisi za Mradi wa
Viongozi wa Afrika wa Kudhibiti Malaria (ALMA) tarehe 18 Julai, 2012 na
siku hiyo hiyo Mhe. Sirleaf atatoa Mhadhara katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam kuhusu “The Role of Women in African Development”.
Vile vile, tarehe 19 Julai, 2012 Mhe. Sirleaf atatembelea Kiwanda
cha Kutengeneza Vyandarua cha A to Z kilichopo Arusha kabla ya kuondoka
siku hiyo hiyo kurejea nchini kwake.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.
16 july 2012







0 comments:
Post a Comment