MAISHA YA UWOYA AIBU TUPU
Uwoya akicheza na Steve Nyerere.
Akiwa na mwanaume.
Shakoor Jongo na Imelda Mtema
MAISHA ya mwigizaji staa wa sinema za Bongo, Irene Uwoya bila kuwa na mumewe, Hamad Ndikumana 'Katauti' yanaonekana kuwa ya aibu tupu kufuatia siku za karibuni kubadilika tabia, hasa kwenye eneo la kujiheshimu, Amani linashuka sasa. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili siku za karibuni umegundua kuwa mambo mengi ya aibu ambayo staa huyo anayafanya, yanasababishwa na kutengana na mumewe ambaye kwa sasa amerudi kwao, Rwanda. “Yaani Uwoya sasa hivi hana tofauti na msichana ambaye hafikirii kuolewa, amechangamka kila idara, hajali cha ndoa wala mume, anaonekana anajipongeza kwa ndoa yake kuvunjika,” alisema rafiki wa karibu wa Uwoya. Tabia nyingine ambayo imegundulika kuwa staa huyo anayo kwa sasa ni kujiachia na waume za watu pamoja na waigizaji wenzake wa kiume huku ikidaiwa hachagui mahala popote yeye ni ‘kambi’. “Siku hizi Uwoya anaweza kukaa sehemu, akamuegemea mwanaume ambaye ni mume wa mtu au akamfanyia msanii mwenzake vitendo ambavyo kwa mtu kama yeye aliye kwenye ndoa hatakiwi kuvifanya (angalia picha ukurasa wa mbele), hata kama ndoa yenyewe ilivunjika,” aliendelea kuanika rafiki huyo. Akaendelea: Lakini bwana hata hao wanaume wenyewe wangekuwa wanaangalia; ya nini kuchezeana na msanii ambaye siku ikifika, mkatoka magazetini mnapiga kelele kulalamika?” Rafiki huyo akaongeza: “Mabadiliko mengine ambayo Uwoya anaonekana kuwa nayo ni mavazi ambapo inadaiwa licha ya kuzoeleka kwa kuvaa mavazi ya nusu utupu akiwa na mumewe lakini kwa sasa amezidisha, anaweza kuvaa kigauni kifupi hadi akikaa nguo ya ndani inaonekana (picha ya aina hiyo iliwahi kutoka kwenye gazeti dada na hili, Ijumaa). Mbali na mavazi, kujiachia na wanaume hadharani, imebainika kuwa, kwa sasa mwigizaji huyo ndiye anayeongozwa kwa kutetwa na marafiki zake wa karibu, wengi wakionesha kutomuunga mkono kufuatia kitendo chake cha kukubali ndoa yake ivunjike. Hilo lilionekana hivi karibuni alipotinga kwenye Hotel Hyatt Kilimanjaro Kempinski, jijini Dar es Salaam ambapo staa mwenzake, Wema Sepetu alikuwa akizindua filamu ya Superstar. Uwoya alitinga ukumbini akiwa amevaa vazi jeusi na la ajabu, chini alivaa soski nyeusi tu bila viatu huku kucha za vidole vya mikononi zikiwa ndefu na kupakwa rangi nyekundu hivyo kuonekana kama mtu wa kwenye filama za kutisha (angalia picha ukurasa wa mbele). “Hivi Irene amevaaje leo jamani? Ina maana kutoka moyoni ameona vile ni sawa?” alisikika akihoji mmoja wa mastaa wa kike Bongo. Hata hivyo, Uwoya alipopigiwa simu juzi, Jumanne, hakupatikana
DIAMOND, WEMA WANASWA HOTELINI
Gari la Wema likiwa eneo la hoteli ya Giraffe.
Gari la Diamond likiwa nje ya hoteli hiyo.
Musa Mateja na Imelda Mtema
NDIVYO ilivyokuwa, staa mkali wa filamu Bongo, Wema Sepetu na mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa yupo juu, Nasibu Abdul a.k.a Diamond ‘Plantinum’ wamenaswa katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano Giraffe iliyopo Mbezi, jijini Dar es Salaam. MESEJI YA KWANZA KWENYE SIMU YA PAPARAZI Asubuhi ya Juni 26, 2012, ujumbe mfupi wa maneno (sms) uliingia kwenye simu ya paparazi wetu ukidondosha madai mazito kuwa, mastaa hao waliowahi kuwa wachumba na baadaye kumwagana kinomanoma, wako kwenye hoteli hiyo ‘wakiponda raha kwani kufa kwaja’. Meseji hiyo ikafafanua: “Tena wapo toka jana, Wema yeye yupo toka alipomaliza ile shughuli yake na Omotola yule mdada wa Naijeria (Nigeria).” MAPAPARAZI WAINGIA MZIGONI Baada ya kupata ujumbe huo, waandishi wetu walikaa kama kamati mbele ya mhariri wao, wakaandaa zana mbalimbali zikiwemo kamera na vifaa vya kurekodia kwa ajili ya kufuatilia ukweli wa meseji hiyo. GARI LA DIAMOND NJE YA HOTELI Waandishi wetu walifika hotelini hapo saa 3:46 ambapo nje ya hoteli hiyo, mapaparazi hao walianza kuamini Platinum yupo ndani baada ya kuliona gari lake aina ya Toyota Prado, lakini katika kuzungusha makengeza yao hawakuweza kulitia machoni gari la Wema. MBELE YA MAPOKEZI YA HOTELI Mbele ya kaunta ya mapokezi, waandishi waliomba kuonana na Wema Sepetu. Mtu wa Mapokezi: Nimwambie nani? Musa: Mwambie baby wake. Mtu wa Mapokezi: Baby wake yupi? Musa: Musa Mateja. Mtu wa Mapokezi alimtwangia simu Wema ambapo alipoambiwa ni Musa Mateja aliamuru asubiri eneo hilo mpaka atakapoitwa kwenda chumbani. DIAMOND HUYO! Waandishi wakiwa wamepiga kambi wakisubiri kuitwa, ghafla Diamond alishuka akiwa mbiombio kuelekea kwenye gari lake kama mtu anayewahi. Mapaparazi wetu walimfuata hadi kwenye gari ambapo alikuwa ameshaingia. MSIKIE ALICHOSEMA Bila kupoteza muda alisomewa mashitaka yake ‘eituzedi’ ambapo alivuta pumzi kwa nguvu kisha akafunguka: “Mimi hata sijui kama Wema yupo hapa hotelini, kwani yupo hapa? Chumba namba ngapi? Mimi nilikuja kwenye mambo yangu, kwa sasa natunga mashairi ya wimbo mwingine kwa hiyo nilikuja tangu jana ili kufanya kazi yangu kwa ufanisi, unajua napenda kuwa sehemu yenye utulivu mkubwa. “Unajua nini, nilikuwa Morogoro, nimerudi jana, nikaja hapa kumfuata Jeff, si unajua yule mshikaji wangu sana? Kuna wakati pia huwa nakuja pale kwenye hoteli moja ipo jirani na ofisini zenu, pale napo pazuri sana, nimewahi kulala. Ha! Ha! Ha! Musa bwana!” MENEJA WA WEMA Meneja wa Wema, Martin Kadinda naye alikutana na waandishi wetu ambapo alishtuka kumwona Diamond kwenye gari lake. Martin: Khaa! Diamond unaweza kuja hapa hotelini halafu unaondoka usinitafute wakati unajua mimi nipo na tuna ishu yetu? Diamond: (kicheko tu). WAANDISHI WARUDI MAPOKEZI, WAITWA KWA WEMA Baada ya kumalizana na Diamond waandishi wetu walirudi mapokezi ambapo walipelekwa kwenye chumba alichomo supastaa mwenye chemchemi za skendo Bongo, Wema na kumkuta akiwa na rafiki yake kipenzi (lakini asiyekubalika na mama yake), Snura Mushi. Wema, baada ya kusomewa mashitaka yake alishtuka sana na kuonesha mshangao kusikia Diamond alilala hotelini hapo. Alisema kuwa yeye ndiyo kwanza yuko kitandani na alikuwa amelala na Snura, habari ya Diamond kuwepo hotelini hapo anasikia kutoka kwa mapaparazi lakini yeye hajui chochote. “Jamani mnavyoniona mimi hapa ndiyo kwanza nimeamka, hata nje sijatoka na watu wa kwanza kuongea nao ni nyinyi, mimi sijui kabisa kama huyo mtu yuko hapa. Kwanza alifuata nini hapa jamani?” Amani: Sisi tulivyosikia alikuwa na wewe, sasa wewe tena unatuuliza sisi, tutajua vipi? Si ndiyo maana tumekuja? Wema: Jamani kusema kweli… (akachukua simu na kumpigia mwanaume aliyedai ni mpenzi wake) dady, wamekuja waandishi hapa wanasema wamesikia nimelala na Diamond, we si tumeongea hadi usiku sana? MASWALI MAGUMU Inawezekana Diamond akafika hotelini hapo bila Wema kuwa na taarifa? Ni kweli kwamba, Wema aliweka kambi pale kwa lengo la kujipumzisha tu akiwa na shoga yake Snura? Utulivu anaodai Diamond aliufuata pale hotelini ulikosekana sehemu nyingine yoyote (hasa nyumbani) ikiwemo ufukweni? Kwa nini Wema aliharakisha kumpigia simu huyo aliyemuita mpenzi wake kumwambia kuhusu waandishi kufuatilia habari ya kulala na Diamond wakati akidai walizungumza hadi usiku sana? UKWELI UPO KWA WEMA, DIAMOND Kwa maelezo yao hayo, bado ukweli unabaki kuwa siri yao. Hata hivyo, penzi halina siri, kama wanaficha, mapaparazi wapo macho kuwafuatilia na kama ni kweli wanatoka, siku moja mambo yatakuwa hadharani.
YALIYOJIRI KWENYE UZINDUZI WA MSIMU WA PILI WA KIPINDI CHA NGOMANI @New Maisha CLub
ELIZABETH GUPTA NDANI YA MOVIE MPYA KUTOKA NIGERIA "THE CARTEL"
NGOMA AFRICA Band KUTUMBUIZA AFRO-RUHR FESTIVAL ,UJERUMANI
DIAMOND AVUTA MKOKO MPYA WA MIL 60
Watoto wafanyiwa unyama gerezani
WATOTO wenye umri chini ya miaka 18 wanaotuhumiwa kwa makosa
mbalimbali au waliohukumiwa huwekwa sehemu moja na watu wazima katika
Gereza la Segerea, Dar es Salaam na baadhi yao kuingiliwa kinyume na
maumbile na kuharibiwa vibaya.
Tuhuma hizo nzito dhidi ya
magereza zilibainika wakati Kamati ndogo ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi,
ilipokuwa ikiwasilisha kwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
inayoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kile
ilichokiona katika gereza hilo baada ya kufanya ziara.
Kamati
hiyo ilitoa taarifa yake katika kikao kilichofanyika Ofisi Ndogo za
Bunge, Dar es Salaam wiki iliyopita ambacho pia kilihudhuriwa na maofisa
mbalimbali wa Jeshi la Magereza akiwemo Kamishna wake Mkuu, Augustino
Nanyaro.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kuwa Kamati
hiyo ya Ukimwi ilieleza kwamba watoto chini ya miaka 18 wanaofika katika
gereza hilo kwa makosa mbalimbali, utambulisho wao huonyesha kuwa wana
miaka 19 hadi 20.
Taarifa hizo zilidai kwamba watoto hao ambao
hukaa na wakubwa mchana, usiku huhamishiwa sehemu nyingine na kuingiliwa
kinyume na maumbile kutokana na mazingira yalivyo ya kukosa pa
kukimbilia.“Waligundua mengi sana, walisema kuwa watoto hao wengi
wameharibika sehemu zao za siri. Kutokana na hali hiyo wanaowafanyia
vitendo hivyo huwatumia pia kuingiza simu, sigara, bangi na dawa za
kulevya gerezani. Wanaingiza vitu hivyo kwa kutumia sehemu zao za siri
zilizoharibiwa,” kilisema chanzo cha habari kutoka kamati hiyo na
kuongeza:
“Unajua huwa wameharibika kwa hiyo sehemu zao huwa wazi
na kubwa kiasi kwamba ni rahisi kuficha simu, bangi, sigara na dawa za
kulevya bila kujulikana.”
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Rosweeter Kasikila alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo alisema katika
kikao hicho walipendekeza wakubwa kutengwa na watoto na kushauri
upelelezi wa kesi kufanywa mapema ili kupunguza msongamano wa
watuhumiwa.
“Hali siyo nzuri yaani sehemu ya kuwekwa watu 40
wanawekwa watu 180. Jambo ambalo hatukulipenda ni jinsi watoto
walivyokuwa wakiwekwa sehemu moja na watu wazima kwa sababu hujifunza
mambo mengi ambayo si mazuri kwa umri wao” alisema Kasikila.
Alisema
kitendo cha watoto kukaa sehemu moja na watu wazima ndicho
kinachosababisha hata kufanyiwa vitendo vichafu ikiwa ni pamoja na
kuingiliwa kinyume na maumbile.“Tulieleza wazi kwamba watoto wanatakiwa
kutengewa sehemu yao kwa sababu wakiwa wao wenyewe si rahisi kufanyiwa
vitendo hivyo,” alisema Kasikila.
Kwa mujibu wa chanzo chetu,
katika kikao hicho maofisa wa magereza walipoulizwa kuhusu umri wa
watoto hao walisema jambo hilo lipo ila hushindwa kufanya lolote kwa
kuwa vielelezo vinavyoletwa huonyesha kuwa umri wao umezidi miaka 18.
Habari zaidi zilieleza kwamba maofisa hao walisema hali hiyo inatokana na mfumo uliopo na kwamba unatakiwa kufanyiwa kazi.
Naibu
Kamishna wa Magereza, Fidelis Mboya alipoulizwa kuhusu hali hiyo, licha
ya kukiri, alisema asingependa kueleza kwa undani mpaka apelekewe
maswali kwa maandishi.
“Nitumie maswali kwa maandishi ili na mimi
nijibu kwa maandishi, hili jambo ni ‘very sensitive’ (nyeti sana), lete
maswali nitakujibu kwa maslahi ya taifa,” alisema Mboya.
Matukio ya utata wa umri
Suala
la umri wa watuhumiwa na hata wafungwa limekuwa gumzo katika siku za
hivi karibuni baada ya mawakili wa mwigizaji wa filamu, Elizabeth
Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii
mwenzake Steven Kanumba, kuwasilisha ombi lao Mahakama Kuu ikitaka
iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto kwa
madai kuwa mteja wao bado ni mtoto.
Uamuzi huo ulikuja baada ya awali, kugonga mwamba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Lakini,
tayari katika Bkutano wa Bunge la Aprili 14, 2010 aliyekuwa Mbunge wa
Viti Maalumu (CUF), Mgeni Jadi Kadika wakati akiuliza swali alitaka
kujua Serikali haioni kuwa kuna ulazima watoto kujengewa magereza yao au
kuwekwa sehemu maalumu.
Alisema hilo linatakiwa kufanyika kwa
kuwa watoto hao wanapokuwa gerezani hukutana na wafungwa wenye tabia
mbalimbali kama wizi, ubakaji, ujambazi na kwamba watoto hao wanaweza
kuiga tabia hizo.
Akijibu swali hilo aliyekuwa Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki alisema kwa mujibu wa Sheria
zinazoratibu, kuongoza na kusimamia masuala ya mahabusu, wafungwa watoto
wanapopelekwa magerezani wanapaswa kutenganishwa na wakubwa.
Kagasheki
alinukuu Kanuni za Uendeshaji wa Jeshi la Magereza (The Prisons
Standing Orders) ya 2003, Kifungu Namba 502, vifungu vidogo vya (ii) na
(iii), wafungwa watoto wanapopelekwa magerezani wanatenganishwa na
wafungwa wakubwa
KUSHADIDI HARAKATI ZA KIJESHI LA UTAWALA WA KIZAYUNI NCHINI LEBANON
Hivi karibuni habari za kushadidi chokochoko za jeshi la utawala ghasibu wa Israel na ukiukaji wake wa mipaka ya Lebanon zimekuwa zikitangazwa na vyombo vya habari. Sambamba na kufanyika maneva ya wanajeshi wa Israel katika maeneo ya mashamba ya Shab’a ya Lebanon yanayokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu, helikopta za utawala huo zimekiuka pia anga ya nchi hiyo. Duru za habari nchini Lebanon zimeripoti kuwa, wanajeshi wa utawala wa Israel wameanza maneva kubwa ya kijeshi katika maeneo ya kusini mwa mashamba hayo ya Shab’a, ambayo yanavishirikisha vikosi vya kutembea kwa miguu na magari ya deraya. Sambamba na kuanza kwa maneva hayo, ndege za kijasusi zisizo na rubani na helikopta za utawala huo zimetanda katika anga ya Shab’a, Golan na vijiji vingine vilivyo mpakani mwa Lebanon. Aidha wakati maneva hayo yanafanyika katika maeneo ya Shab’a, habari zinaripoti kuwepo kundi kubwa la vikosi vya utawala huo vinavyopiga doria katika maeneo hayo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel. Kuongezeka hatua za kichokozi na uwezekano wa utawala huo wa Kizayuni kuanzisha tena vita nchini Lebanon ni jambo linaloweza kujadiliwa kwa mitazamo tofauti. Utawala wa Kizayuni unashadidisha hatua za kijeshi katika maeneo unayoyakalia kwa mabavu huko Lebanon ili baadaye uweze kuandaa uwanja wa kujitanua katika maeneo hayo. Hii ni katika hali ambayo sisitizo la wananchi wa Lebanon la kutaka kurejeshwa maeneo yote ya nchi hiyo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel limeutia kiwewe utawala huo kwa kuchelea kwamba, kushadidi muqawama wa wananchi kutaupelekea uondoke katika maeneo mengine uliyoyapora.
Mwaka 2000 Utawala wa Israel ulilazimika kurejea nyuma na kuondoka katika baadhi ya maeneo uliyokuwa ukiyakalia kwa mabavu baada ya kupata kipigo mtawalia kutoka kwa wanamapambano wa Harakati ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah. Katika kufunika aibu ulioipata kufuatia kipigo hicho, utawala huo ungali unayakalia kwa mabavu maeneo mengine ya nchi hiyo hadi leo.
Kuongezeka mielekeo ya kupinga utawala wa Kizayuni Mashariki ya Kati baada ya kudhihiri mwambo wa Kiislamu katika eneo, kumezidisha wasiwasi wake na kuufanya uhofu kwamba wimbi jipya la upinzani dhidi yake linaweza kuzuka katika eneo. Kwa ajili hiyo utawala huo ghasibu umezidisha hatua zake za kijeshi kwa lengo la kuimarisha nafasi yake katika maeneo unayoyakalia kwa mabavu na wakati huohuo kudhihirisha nguvu zake bandia kwa shabaha ya kuzusha khofu na kuwatisha wananchi wa Lebanon wasije wakaunga mkono mapambano dhidi yake. Katika upande wa pili, madola ya Magharibi yanatekeleza njama tofauti za kudhoofisha uwezo wa muqawama ambao ni tishio kubwa kwa utawala ghasibu wa Israel, kwa kuvuruga amani na uthabiti wa nchi za Syria na Lebanon. Ni kwa ajili hiyo ndipo madola hayo yakiongozwa na Marekani yakajaribu kuzitumbukiza Lebanon na Syria katika hali ya mchafukoge na vita vya ndani ili hatimaye yapate kuingilia na kuzidhibiti nchi mbili hizo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni
SEAN PAUL AMUOA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI
Staa huyo wa ngoma ya Got 2 Luv You amefunga pingu za maisha na Stewart kwa bonge la harusi kwenye ukumbi wa Boone Hall Oasis nchini Jamaica.
Sean Paul, ambaye jina lake ni Sean Paul Henriques, anadaiwa kumchumbia mpenzi wake kwenye sherehe ya mwaka mpya wa 2011.
Wapenzi hao waliokuwa na uhusiano tangu mwaka 2002, wamefunga ndoa mbele ya ndugu na jamaa kwenye harusi hiyo iliyokuwa ya watu maalum tu na ulinzi mkali.
Baada ya kufunga ndoa Sean Paul na Stewart ambaye ni mtangazaji maarufu wa TV nchini Jamaica walielekea French Polynesia kwa ajili ya honeymoon
JUSTIN BIEBER APIGA SHOW YA BURE NCHINI MEXICO
DOGO JANJA ATUIWA VIRAGO TIP TOP CONNECTION
Akizumngumza na Teentz .com mapema leo kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’ amesema kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila siku badala yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya kurudi kwao na wakati huo tulifanya mawasiliano na



































