THE BEST BLOG IN TOWN

Powered by Blogger.

Text

RSS

KUSHADIDI HARAKATI ZA KIJESHI LA UTAWALA WA KIZAYUNI NCHINI LEBANON


Hivi karibuni habari za kushadidi chokochoko za jeshi la utawala ghasibu wa Israel na ukiukaji wake wa mipaka ya Lebanon zimekuwa zikitangazwa na vyombo vya habari. Sambamba na kufanyika maneva ya wanajeshi wa Israel katika maeneo ya mashamba ya Shab’a ya Lebanon yanayokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu, helikopta za utawala huo zimekiuka pia anga ya nchi hiyo. Duru za habari nchini Lebanon zimeripoti kuwa, wanajeshi wa utawala wa Israel wameanza maneva kubwa ya kijeshi katika maeneo ya kusini mwa mashamba hayo ya Shab’a, ambayo yanavishirikisha vikosi vya kutembea kwa miguu na magari ya deraya. Sambamba na kuanza kwa maneva hayo, ndege za kijasusi zisizo na rubani na helikopta za utawala huo zimetanda katika anga ya Shab’a, Golan na vijiji vingine vilivyo mpakani mwa Lebanon. Aidha wakati maneva hayo yanafanyika katika maeneo ya Shab’a, habari zinaripoti kuwepo kundi kubwa la vikosi vya utawala huo vinavyopiga doria katika maeneo hayo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel. Kuongezeka hatua za kichokozi na uwezekano wa utawala huo wa Kizayuni kuanzisha tena vita nchini Lebanon ni jambo linaloweza kujadiliwa kwa mitazamo tofauti. Utawala wa Kizayuni unashadidisha hatua za kijeshi katika maeneo unayoyakalia kwa mabavu huko Lebanon ili baadaye uweze kuandaa uwanja wa kujitanua katika maeneo hayo. Hii ni katika hali ambayo sisitizo la wananchi wa Lebanon la kutaka kurejeshwa maeneo yote ya nchi hiyo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel limeutia kiwewe utawala huo kwa kuchelea kwamba, kushadidi muqawama wa wananchi kutaupelekea uondoke katika maeneo mengine uliyoyapora.
Mwaka 2000 Utawala wa Israel ulilazimika kurejea nyuma na kuondoka katika baadhi ya maeneo uliyokuwa ukiyakalia kwa mabavu baada ya kupata kipigo mtawalia kutoka kwa wanamapambano wa Harakati ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah. Katika kufunika aibu ulioipata kufuatia kipigo hicho, utawala huo ungali unayakalia kwa mabavu maeneo mengine ya nchi hiyo hadi leo.
Kuongezeka mielekeo ya kupinga utawala wa Kizayuni Mashariki ya Kati baada ya kudhihiri mwambo wa Kiislamu katika eneo, kumezidisha wasiwasi wake na kuufanya uhofu kwamba wimbi jipya la upinzani dhidi yake linaweza kuzuka katika eneo. Kwa ajili hiyo utawala huo ghasibu umezidisha hatua zake za kijeshi kwa lengo la kuimarisha nafasi yake katika maeneo unayoyakalia kwa mabavu na wakati huohuo kudhihirisha nguvu zake bandia kwa shabaha ya kuzusha khofu na kuwatisha wananchi wa Lebanon wasije wakaunga mkono mapambano dhidi yake. Katika upande wa pili, madola ya Magharibi yanatekeleza njama tofauti za kudhoofisha uwezo wa muqawama ambao ni tishio kubwa kwa utawala ghasibu wa Israel, kwa kuvuruga amani na uthabiti wa nchi za Syria na Lebanon. Ni kwa ajili hiyo ndipo madola hayo yakiongozwa na Marekani yakajaribu kuzitumbukiza Lebanon na Syria katika hali ya mchafukoge na vita vya ndani ili hatimaye yapate kuingilia na kuzidhibiti nchi mbili hizo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment