WATOTO wenye umri chini ya miaka 18 wanaotuhumiwa kwa makosa
mbalimbali au waliohukumiwa huwekwa sehemu moja na watu wazima katika
Gereza la Segerea, Dar es Salaam na baadhi yao kuingiliwa kinyume na
maumbile na kuharibiwa vibaya.
Tuhuma hizo nzito dhidi ya
magereza zilibainika wakati Kamati ndogo ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi,
ilipokuwa ikiwasilisha kwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
inayoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kile
ilichokiona katika gereza hilo baada ya kufanya ziara.
Kamati
hiyo ilitoa taarifa yake katika kikao kilichofanyika Ofisi Ndogo za
Bunge, Dar es Salaam wiki iliyopita ambacho pia kilihudhuriwa na maofisa
mbalimbali wa Jeshi la Magereza akiwemo Kamishna wake Mkuu, Augustino
Nanyaro.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kuwa Kamati
hiyo ya Ukimwi ilieleza kwamba watoto chini ya miaka 18 wanaofika katika
gereza hilo kwa makosa mbalimbali, utambulisho wao huonyesha kuwa wana
miaka 19 hadi 20.
Taarifa hizo zilidai kwamba watoto hao ambao
hukaa na wakubwa mchana, usiku huhamishiwa sehemu nyingine na kuingiliwa
kinyume na maumbile kutokana na mazingira yalivyo ya kukosa pa
kukimbilia.“Waligundua mengi sana, walisema kuwa watoto hao wengi
wameharibika sehemu zao za siri. Kutokana na hali hiyo wanaowafanyia
vitendo hivyo huwatumia pia kuingiza simu, sigara, bangi na dawa za
kulevya gerezani. Wanaingiza vitu hivyo kwa kutumia sehemu zao za siri
zilizoharibiwa,” kilisema chanzo cha habari kutoka kamati hiyo na
kuongeza:
“Unajua huwa wameharibika kwa hiyo sehemu zao huwa wazi
na kubwa kiasi kwamba ni rahisi kuficha simu, bangi, sigara na dawa za
kulevya bila kujulikana.”
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Rosweeter Kasikila alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo alisema katika
kikao hicho walipendekeza wakubwa kutengwa na watoto na kushauri
upelelezi wa kesi kufanywa mapema ili kupunguza msongamano wa
watuhumiwa.
“Hali siyo nzuri yaani sehemu ya kuwekwa watu 40
wanawekwa watu 180. Jambo ambalo hatukulipenda ni jinsi watoto
walivyokuwa wakiwekwa sehemu moja na watu wazima kwa sababu hujifunza
mambo mengi ambayo si mazuri kwa umri wao” alisema Kasikila.
Alisema
kitendo cha watoto kukaa sehemu moja na watu wazima ndicho
kinachosababisha hata kufanyiwa vitendo vichafu ikiwa ni pamoja na
kuingiliwa kinyume na maumbile.“Tulieleza wazi kwamba watoto wanatakiwa
kutengewa sehemu yao kwa sababu wakiwa wao wenyewe si rahisi kufanyiwa
vitendo hivyo,” alisema Kasikila.
Kwa mujibu wa chanzo chetu,
katika kikao hicho maofisa wa magereza walipoulizwa kuhusu umri wa
watoto hao walisema jambo hilo lipo ila hushindwa kufanya lolote kwa
kuwa vielelezo vinavyoletwa huonyesha kuwa umri wao umezidi miaka 18.
Habari zaidi zilieleza kwamba maofisa hao walisema hali hiyo inatokana na mfumo uliopo na kwamba unatakiwa kufanyiwa kazi.
Naibu
Kamishna wa Magereza, Fidelis Mboya alipoulizwa kuhusu hali hiyo, licha
ya kukiri, alisema asingependa kueleza kwa undani mpaka apelekewe
maswali kwa maandishi.
“Nitumie maswali kwa maandishi ili na mimi
nijibu kwa maandishi, hili jambo ni ‘very sensitive’ (nyeti sana), lete
maswali nitakujibu kwa maslahi ya taifa,” alisema Mboya.
Matukio ya utata wa umri
Suala
la umri wa watuhumiwa na hata wafungwa limekuwa gumzo katika siku za
hivi karibuni baada ya mawakili wa mwigizaji wa filamu, Elizabeth
Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii
mwenzake Steven Kanumba, kuwasilisha ombi lao Mahakama Kuu ikitaka
iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto kwa
madai kuwa mteja wao bado ni mtoto.
Uamuzi huo ulikuja baada ya awali, kugonga mwamba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Lakini,
tayari katika Bkutano wa Bunge la Aprili 14, 2010 aliyekuwa Mbunge wa
Viti Maalumu (CUF), Mgeni Jadi Kadika wakati akiuliza swali alitaka
kujua Serikali haioni kuwa kuna ulazima watoto kujengewa magereza yao au
kuwekwa sehemu maalumu.
Alisema hilo linatakiwa kufanyika kwa
kuwa watoto hao wanapokuwa gerezani hukutana na wafungwa wenye tabia
mbalimbali kama wizi, ubakaji, ujambazi na kwamba watoto hao wanaweza
kuiga tabia hizo.
Akijibu swali hilo aliyekuwa Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki alisema kwa mujibu wa Sheria
zinazoratibu, kuongoza na kusimamia masuala ya mahabusu, wafungwa watoto
wanapopelekwa magerezani wanapaswa kutenganishwa na wakubwa.
Kagasheki
alinukuu Kanuni za Uendeshaji wa Jeshi la Magereza (The Prisons
Standing Orders) ya 2003, Kifungu Namba 502, vifungu vidogo vya (ii) na
(iii), wafungwa watoto wanapopelekwa magerezani wanatenganishwa na
wafungwa wakubwa
Watoto wafanyiwa unyama gerezani
9:01 AM |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 comments:
Post a Comment