Hatimaye supastaa wa dancehall nchini Jamaica Sean Paul amemuoa mpenzi wake wa siku nyingi Jodi “Jinx” Stewart.
Staa huyo wa ngoma ya Got 2 Luv You amefunga pingu za maisha na
Stewart kwa bonge la harusi kwenye ukumbi wa Boone Hall Oasis nchini
Jamaica.
Sean Paul, ambaye jina lake ni Sean Paul Henriques, anadaiwa kumchumbia mpenzi wake kwenye sherehe ya mwaka mpya wa 2011.
Wapenzi hao waliokuwa na uhusiano tangu mwaka 2002, wamefunga ndoa
mbele ya ndugu na jamaa kwenye harusi hiyo iliyokuwa ya watu maalum tu
na ulinzi mkali.
Baada ya kufunga ndoa Sean Paul na Stewart ambaye ni mtangazaji
maarufu wa TV nchini Jamaica walielekea French Polynesia kwa ajili ya
honeymoon
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







0 comments:
Post a Comment