THE BEST BLOG IN TOWN

Powered by Blogger.

Text

RSS

NISHA NA MAINDA WADAIWA KUZICHAPA

Salma Jabu ‘Nisha’.
Ruth Suka ‘Mainda’.
  MASTAA wanaowakilisha vyema katika kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ na Ruth Suka ‘Mainda’ wamedaiwa kuzichapa kavukavu.
Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo chetu kilicho karibu na mastaa hao, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, kilisema tukio hilo limetokea mbele ya macho yake, wiki iliyopita Tegeta, jijini Dar es Salaam, ambapo wasanii hao walikuwa wakirekodi filamu.
“Walianza kama utani, walikuwa wanaelekezana kitu, tena katikati ya kurekodi, lakini ghafla wakaanza kubishana hadi kufikia hatua ya kukamatana...hasira zikampanda Mainda na kuzimia,” kilieleza chanzo hicho.
Nisha alipopatikana kwa njia ya simu na kutakiwa kuzungumzia suala hilo, alikiri kuwa na Mainda na wasanii wengine Tegeta, wakirekodi filamu lakini aliruka kupigana naye, achilia mbali Mainda kuzimia.
“Jamani siwezi kugombana na Mainda, kwanza ni rafiki yangu sana. Kama huyo mtu anasema tuligombana itakuwa ni kwenye hiyo filamu lakini si vinginevyo.”
Mainda alisema: “Mh! Jamani wewe hizo habari umezipata kwa nani? Kuchapana hatujachapana labda kutofautina kwa kawaida ambayo hiyo inatokea kwa mtu yoyote hasa katika kazi kama tuliyokuwa tunaifanya.”

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment